Consular Matters

Travel documents

文字バー

| Passport Application Utaratibu wa kuomba pasipoti mpya
| Emergency Travel Document (ETD) Hati ya Dharura ya Safari (ETD)

PROCEDURES FOR APPLICATION OF NEW PASSPORTS

Procedures for application of new passports through Embassies are as follows:

 1. All new passports will be issued at the Immigration Department Headquarters in Dar es Salaam and in Zanzibar.

 2. The application for a new passport should be submitted at the Embassy by the applicant him/herself.
  The Embassy has been delegated to process all applications from holders of old authentic Tanzanian passports.

 3. The Embassy will then send the completed application forms, relevant documents and passport fee to the Immigration Headquarters for the issuance of new passports.
  The Immigration Headquarters will then send the new passports to the relevant applicants through the Embassy.

 4. Passport fee

  • Application forms・・・US$10 each
  • Passport fee・・・US$40

  Applicants in Japan are required to pay in Japanese Yen, which is equivalent to 50 US$.
  Fee varies depending on the rate.
  It should be noted that the applicant would be required to re-pay for any replacement of the application form.
  Hence, accuracy should be observed during the process of filling the forms.

 5. Application forms

  The application forms are available at the Chancery.

  You are advised to visit the Embassy Homepage to download the form, study and understand the contents and prepare all the necessary information.

  The original application form will be issued by the Passport Officer during the meeting with him/her at the Embassy.

  ●Passport Application Form Download (PDF)

  The applicant will be required to sign the properly filled application form in presence of a Passport Officer using a special designated pen and his/her fingerprints will be taken.

 6. Photo

  The applicant is required to submit 5 passport size photos with a light blue background.
  The recommended size is 4.5cm × 4.0 cm.

 7. The applicant is also required to submit his/her previous passport for verification, together with copies of page 1 - 4, last page that shows the Dossier Number, the page with visa/permit and a copy of a his/her resident permit.

 8. Other documents to be submitted are indicated on the application form.
  Please submit them if you didn't submit during the application of your previous passport.

 9. The applicant will be allowed to retain his/her previous passport during the processing of the new passport.
  However, he/she will be asked to submit it to the Embassy through registered mail for cancellation when the new passport arrives.
  The Embassy will then send the new and the cancelled passport to the bearer.

 10. Child endorsement in the passport

  Kindly note that there is no endorsement of children in the passports any more.
  Every Tanzanian citizen is required to have her/his own passport.
  When making passport applications for the first time, you need to have an original birth certificate and produce a copy for certification.
  Other requirements and procedures are same as above.

 11. Replacement of lost passport

  Applicant who has lost his/her passport is required to submit a police report and a proof of an advertisement in the local newspaper on the same, as well as a letter addressed to the Commissioner-general of Immigration Services stating in detail reasons for loss of passport.
  For the first lost case the passport fee cost double of the normal one (US$ 100 or equivalent in Yen) and for the second lost case is three times (i.e. US$ 150 or equivalent in Yen).
  The applicant will also follow the same procedures as it is listed above.

 12. Change of name in the passport

  For anyone who wishes to change his/her name for any reason such as marriage, etc., he/she will be required to submit new application, which will bear the new name.
  In addition to normal documents that are enclosed during the application of new passport, they need to submit a supporting document on change of name (from lawyer, marriage certificate etc.).

UTARATIBU WA KUOMBA WA PASIPOTI MPYA

Utaratibu wa kuomba pasipoti mpya kupitiaUbalozini ni kama ifuatavyo:-

 1. Uandikaji wa pasipoti zote unafanywa na Makao Makuu ya Uhamiaji Dar es Salaam, pamoja na Zanzibar.

 2. Mwombaji anatakiwa kuwasilisha maombi ya pasipoti Ubalozini yeye binafsi.
  Ubalozi utashughulikia na kuidhinisha maombi ya pasipoti kwa raia wa Tanzania walio na pasipoti za zamani zilizo halali.

 3. Ubalozi utatuma maombi hayo Makao Makuu kwa Mkurugenzi wa Uhamiaji.
  Baada ya Uhamiaji kutayarisha pasipoti, itazituma Ubalozini ili ziwasilishwe kwa wahusika.

 4. Ada ya pasipoti

  • Fomu za maombi ya pasipoti・・・US$10
  • Pasipoti italipiwa ・・・US$40

  Izingatiwe kwamba, iwapo mwombaji wa pasipoti atajaza vibaya, ataharibu au kuchafua fomu ya maombi, atalazimika kununua/kulipia fomu nyingine kwa US$ 10.

 5. Fomu za maombi:

  Fomu za maombi zinapatikana Ubalozini.
  Mwombaji anashauriwa kutembelea tovuti ya Ubalozi ili kusoma maelezo ya fomu hiyo na kuandaa taarifa zote muhimu na vitu vinavyotakiwa kuwasilishwa wakati wa kuomba pasipoti mpya.
  Fomu halisi itajazwa wakati atakapoonana na Afisa wa Pasipoti..

  ●Pata fomu ya maombi ya pasipoti (PDF)

  Mwombaji wa pasipoti akishajaza fomu ya maombi, ataweka sahihi yeye mwenyewe mbele ya afisa wa pasipoti/Ubalozi kwa kutumia kalamu maalumu.
  Aidha mwombaji huyo atachukuliwa alama za vidole na afisa wa pasipoti/Ubalozi.

 6. Picha

  Mwombaji wa pasipoti anatakiwa kuwasilisha picha tano(5) za pasipoti zenye rangi bluu bahari kwa nyuma(a light blue background).

  Picha hizo ziwe zenye urefu wa 4.5 sentimeta na upana wa 4.0 sentimeta(4.5×4.0 cm).

 7. Mwombaji atatakiwa kuambatanisha maombi yake na pasipoti aliyokuwa nayo kwa ajili ya kuithibitisha, pamoja na nakala za ukurasa wa 1 - 4, ukurasa wa mwisho wenye namba ya faili, ukurasa wenye visa au kibali cha kuishi mahali alipo (resident permit) pamoja na nakala ya "Certificate of Alien Registration" kwa wale waishio Japan.

 8. Hati nyingine zinazotakiwa kuambatanishwa na maombi ya pasipoti ni kama ilivyoorodheshwa katika fomu za maombi.
  Mwombaji anapaswa kuwasilisha hati hizo ikiwa hakuwa ameziwasilisha katika maombi ya pasipoti ya zamani.

 9. Mwombaji ataruhusiwa kubaki na pasipoti yake mpaka hapo pasipoti mpya itakapotumwa Ubalozini.
  Akishaarifiwa kuwasili kwa pasipoti yake, mwombaji ataituma pasipoti ya zamani kwa "Registered mail", ili iweze kufutwa na kisha kurudishwa kwake ikiambatanishwa na pasipoti mpya.

 10. Kuingiza majina ya watoto katika pasipoti:

  Utaratibu wa kuingiza majina ya watoto kwenye pasipoti ya mzazi hautumiki tena.
  Kila Mtanzania - awe mtoto au mtu mzima anapaswa kuwa na pasipoti yake.
  Maombi ya pasipoti kwa ajili ya mtoto yaambatanishwe na nakala ya cheti cha kuzaliwa.
  Cheti halisi pia kiletwe wakati wa kuonana na Afisa anayeshughulikia maombi ya pasipoti kwa ajili ya kukihakiki.
  Taratibu zote zilizoelezwa juu zitafuatwa wakati wa kuwasilisha maombi ya pasipoti kwa ajili ya mtoto.

 11. Pasipoti iliyopotea:

  Mwombaji aliyepoteza pasipoti anatakiwa kuwasilisha maombi ya pasipoti mpya akiambatanisha ripoti ya polisi kuhusu kupotea kwa pasipoti, tangazo la gazeti (gazeti la eneo unaloishi) kuhusu upotevu huo, na barua kwenda kwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji inayoeleza sababu za kupoteza pasipoti.
  Ada ya pasipoti kwa iliyopotea kwa mara ya kwanza ni mara mbili ya gharama ya ada halisi, yaani US$ 100 (au kiasi sawa na hicho kwa Yen) na ada kwa pasipoti iliyopotea kwa mara ya pili ni mara tatu ya gharama ya ada halisi – US$ 150 ( au kiasi sawa na hicho kwa Yen).
  Mwombaji atafuata pia taratibu nyingine za kawaida za maombi ya pasipoti mpya zilizoorodheshwa juu.

 12. Kubadili jina kwenye pasipoti:

  Kwa yeyote anayependa kubadili jina kwenye pasipoti kwa sababu mbalimbali kama kuolewa/kuoa n.k., anatakiwa kujaza fomu za maombi ya pasipoti inayoonyesha jina analotaka kutumia.
  Anatakiwa kuambatanisha maombi hayo na uthibitisho wa kubadili jina (mathalani nyaraka ya kisheria, cheti cha ndoa, n.k.).
  Nyaraka nyingine za kawaida zinazohusiana na maombi ya pasipoti mpya nazo zinatakiwa kuambatanishwa.

EMERGENCY TRAVEL DOCUMENT (ETD)

Emergency Travel Document (ETD) will be issued for Tanzanians who are traveling on emergency reasons.
The ETD can enable them to travel only to Tanzania.
ETD could be issued due to the following reasons:

 • Loss of passport (Please attach a police report on the loss of passport)
 • Repatriation
 • Traveling to Tanzania to process a new passport
 • Traveling to Tanzania on an emergence while waiting for the processing of your passport application.

ETD fee is Yen 3,000

●ETD Application Form Download

Other requirements are;

 • 2 passport sized photos
 • evidence that the applicant is a Tanzanian
 • a police report and newspaper advertisement for lost passport
 • a copy of travel itinerary for those who are traveling to Tanzania

he applicant can send the application by registered mail if he lives far from Tokyo.

When the ETD is processed, it can also be sent to applicant through the same way.
The applicant is responsible for the cost of sending the ETD by registered mail.

HATI YA DHARURA YA SAFARI (EMERGENCY TRAVEL DOCUMENT)

Hati ya Dharura ya Safari (ETD) inatolewa kwa Watanzania wenye sababu kati ya zifuatazo:-

 • Waliopoteza pasipoti (Tafadhali ambatanisha maombi na ripoti ya polisi)
 • Wanaorudishwa nyumbani na mamlaka ya uhamiaji ya nchi wanakoishi
 • Wanaotaka kwenda Tanzania kuomba pasipoti mpya
 • Wenye safari za dharura kwenda Tanzania wakati maombi yao ya pasipoti mpya hayajashughuliwa

Ada kwa ajili ya Hati ya Dharura ya Safari ni Yen 3,000

●Pata fomu ya maombi ya ETD (PDF)

Mwombaji anatakiwa pia kuwasilisha vitu vifuatavyo;-

 • picha mbili (passport size)
 • uthibitisho kuwa ni raia wa Tanzania
 • ripoti ya polisi na tangazo la gazeti kwa aliyepoteza pasipoti
 • na nakala ya utaratibu wa safari (itinerary) kwa anayesafiri kwenda Tanzania

Waombaji wanaoishi mbali na Tokyo wanaweza kutuma maombi yao kwa njia ya posta (registered mail).
Baada ya kutayarisha ETD, Ubalozi utaituma kwa mhusika kwa kutumia njia hiyo hiyo. Gharama za kutuma ETD zitalipwa na mwombaji.